Discussion During The Tanzania Pulses Network Meeting

Siku ya Tarehe 13 Julai 2017 wadau wa Mikunde kunde Tanznaia ambao ni wanachama wa tanzania Pulses network (TPN) kwa support ya VECO Tanzania na ITC-SITA Project tulikuwa na Kikao kizur cha wadau wa Mikunde kunde Tanzania na moja ya mambo tumekubaliana ni Kusajili Mtandao wa Mikunde Kunde Tanzania.

Kwa kipindi cha mwaka.mzima toka Mradi wa Masoko ya Mikunde kunde uanze mwaka 2015, sekretariat ya Mtandao wa mikunde kunde ilikuwa ikitolewa na Barqza la Nafaka Ukanda wa Afrika ya mashariki (EAGC).
Pia wawakilishi wa vikundi vya wakulima, wakulima binafsi, watafiti, wakusanyaji na watoa huduma wa katika mnyororo wa Thamani wa Mikunde kunde (Pulses) wameweza kukutana na kujadilianna kutumia fursa kufikia hitaji la soko kuzingatia ubora, muda na aina.

Makampuni makubwa ya wanunuzi yakiwemo ETG, QPE, EV Exporters, MAVIGA na KILIMO MARKET waliweza kukutana na wawakilishi wa vikundi vya wakulima kutoka Babati, Mtwara, Lindi, Dodoma, Karatu, Shinyanga,Iringa na Mbeya.

Pia wawakilishi kutoka wizara ya Kilimo, Viwanda, na vituo vya utafiti walishiriki.
Ili kufikia malengo ya kusajili Mtandao kamati ya mpito ikiwa na wawakilishi toka TCCIA, EAGC, AMSHA, TGFA, UKIRIGURU ARI, MSU/ASPIRES PROJECT, BAJWA FARMERS, KILIMO MARKET na MAI.